Namna ya ulipaji wa gharama za usafiri — masharti ya Doctor Cargo
Lini kulipa, ni zipi accepted, na nini kinaashiria bei imehakikishwa kabla ya ndege.
Gharama za usafiri wa angani hutegemea uzito wa kutoza, njia (mizigo ya kawaida au hatari), na kipindi cha soko. Hii ni muhtasari wa jinsi tunavyofanya kazi na wateja.
Kabla ya kutuma
Tunakupa quotation iliyo wazi (kwa USD au kama ilivyokubaliwa). Hakuna "surprise" baada ya mzigo kuwasili kwenye warehouse bila taarifa ya mabadiliko ya vipimo.
Malipo
Unaweza kulipa kwa njia zilizokubaliwa na ofisi yetu (TZS, USD, au mpangilio wa RMB kupitia huduma husika). Baada ya malipo ya sehemu au kamili kulingana na makubaliano, tunahifadhi nafasi ya ndege au tunachakata mzigo.
Makato na marejesho
Kama mzigo umeghairiwa kabla ya booking ya ndege, masharti ya kurejesha fedha huonyeshwa kwenye invoice yako. Baada ya ndege kushatengenezwa, marejesho yanategemea hali ya ndege na makubaliano ya kampuni ndege.
Maswali mahususi? Wasiliana nasi kabla ya kulipa supplier nje ya mfumo wetu.